Home Ligi Kuu KOCHA MTIBWA SUGAR ATAJA KINACHOITESA TIMU YAKE

KOCHA MTIBWA SUGAR ATAJA KINACHOITESA TIMU YAKE


 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa shida kubwa iliyopo kwenye kikosi hicho kwa sasa ni kukosa wachezaji wenye uwezo wa kupambana ndani ya dakika 90 na kupata matokeo chanya kwa kuwa wale waliosepa hawakutafutiwa mbadala.

Miongoni mwa nyota ambao wamesepa msimu uliopita Mtibwa Sugar ni pamoja na Dickson Job ambaye alikuwa beki wa kati chaguo la kwanza kwa sasa anakipiga Yanga.

Alipokuwa Mtibwa Sugar kwenye mechi 19 ambazo walikuwa wamecheza wakati ule kabla ya usajili wa dirisha dogo alicheza jumla ya mechi 18 na alikosa mchezo mmoja dhidi ya Mbeya City msimu huu.

Thiery amesema kuwa kuondoka kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza bila kufanya usajili ni tatizo ambalo linawasumbua Mtibwa Sugar.

“Walikuwa na nguvu hapo awali na walikuwa na uwezo wa kufanya vizuri ila pale ambapo wale wachezaji waliokuwa wapo kikosi cha kwanza wameondoka ilikuwa tatizo hapo na kingine ni kwamba hakujafanyika usajili mkubwa.

“Naona kwamba kikosi kitapambana kurudi kwenye uimara wake ila ni mpaka muda kidogo upite kwani hakuna kitu chepesi kwenye maisha ya mpira,” amesema.

Thiery kwa sasa yupo zake Rwanda baada ya kuomba apewe mapumziko kwa muda.

SOMA NA HII  VPL: POLISI TANZANIA 0-1 SIMBA, CCM KIRUMBA