Home Yanga SC YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE,

YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE,


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa una imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho Aprili 30, mbele ya Tanzania Prisons wenye sera ya pira gwaride ambao ni wa Kombe la Shirikisho.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi umeweka kambi kwa muda Mbeya kabla ya kuibukia Songea kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora.

Kikosi hicho kilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru na bao pekee la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Fiston Abdulazack ambaye kwa sasa yupo na kikosi pia.

Nyota wengine ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Ramadhan Kabwili, Farouk Shikahlo na Metacha Mnata kwa upande wa makipa.

Dickson Job na Abdala Shaibu, ‘Ninja’ kwa upande wa mabeki pamoja na Paul Godfrey, ‘Boxer’.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua Tanzania Prisons ni timu ngumu na imara ila watapambana kupata matokeo.

“Katika hali ya kawaida, Tanzania Prisons ni timu imara na inafanya vizuri kwenye mechi zake zote na hata tukikutana nao huwa inakuwa ngumu kupata matokeo ila haina maana kwamba hatuna uwezo wa kupata ushindi kwao.

“Kwa maandalizi ambayo tunayafanya imani yetu tunakwenda kufanya kweli na kutafuta ushindi, mashabiki waendelee kutupa sapoti uwezo na nia ipo,” .

Mchezo wao wa kwanza Yanga kucheza Uwanja wa Nelson Mandela ulikuwa ni wa ligi na walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 hata ule wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Prisons.

SOMA NA HII  HUYU HAPA KIPA WA YANGA REKODI ZINAMBEBA MBELE YA SIMBA