NYOTA wa Azam FC, Prince Dube amezidi kuendeleza kasi ya kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ardhi ya Bongo.
Wakati ubao wa Azam Complex, usiku wa kuamkia leo ukisoma Azam FC 2-0 Biashara United, mshambuliaji huyu aliongeza akaunti yake ya mabao kwa kutupia bao moja.
Bao la pili lilifungwa na kiungo Mudathir Yahaya na kuifanya Azam FC kuzidi kuongeza nguvu katika ufalme wa tatu bora huku kasi ya nyota huyo ikizidi kuwa kubwa.
Kwenye orodha ya watupiaji yeye ni namba moja akiwa na jumla ya mabao 14 anafuatiwa na Meddie Kagere mwenye mabao 11 pamoja na John Bocco mwenye mabao 10 hawa wote wanacheza ndani ya Klabu ya Simba.
Kwenye msimamo, Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa imekusanya jumla ya pointi 60 baada ya kucheza mechi 30 na namba moja ipo mikononi mwa Simba akiwa na poiti 61 baada ya kucheza mechi 25 nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga wenye pointi 61 baada ya kucheza mechi 29.