Home epl ARSENAL YAINYOOSHA NEWCASTLE UNITED

ARSENAL YAINYOOSHA NEWCASTLE UNITED



WAKATI Arsenal ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United,  Uwanja wa St James Park, Mohamed Elneny alifunga bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu England. 

Ilikuwa ni dakika ya sita nyota huyo alipachika bao hilo na kuwafanya Arsenal kuongoza mpaka muda wa mapumziko katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Bao la pili lilipachikwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang ambaye alipachika bao pili kipindi cha pili dakika ya 66.

Ushindi huo unaifanya  Arsenal kufikisha jumla ya pointi 49 ipo nafasi ya 34 na Newcastle United ipo nafasi ya 17 na pointi zake ni 36 kinara ni Manchester City ina pointi 80 ambaye anapewa nafasi za kutwaa taji hilo lililo mikononi mwa Liverpool.


SOMA NA HII  JORGINHO ALIFUNDISHWA SOKA NA MAMA YAKE