Home kimataifa ATLETICO MADRID YATWAA UBINGWA, SUAREZ SHUJAA

ATLETICO MADRID YATWAA UBINGWA, SUAREZ SHUJAA


LUIS Suarez mshambuliaji wa Atletico Madrid alimwaga machozi wakati timu yake hiyo ikitwaa ubingwa wa La Liga baada ya ubao wa Uwanja wa Jose Zorrila kusoma Valladolid 1-2 Ateltico Madrid.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulikuwa ni wa maamuzi ambapo Oscar Pilano alianza kuwatungua Atletico dakika ya 18 na Angelle Correa dakika ya 57 aliweka mzani sawa na dakika ya 67 Suarez alifunga bao la ushindi na kumfanya afunge jumla ya mabao 21 ndani ya La La Liga kwa msimu wa 2020/21.

Suarez nyota wa zamani wa Barcelona alishangazwa na kitendo cha mabosi wa timu hiyo kumfungulia mlango na kumtaka aondoke katika timu hiyo msimu uliopita na aliamua kwenda Atletico Madrid bure kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umekwisha jambo ambalo lilikuwa linamuumiza kwa kuwa alishushwa thamani yake ndani ya Barcelona.

Baada ya mchezo wao wa mwisho na kuthibitishwa kwamba Atletico Madrid ni mabinhwa wa La Liga, Suarez alikuwa mpole na kusema kuwa Barcelona hawakumthamini kwa kuwa walimuondoa licha ya kuwa alikuwa akijituma.

Atletico Madrid imetwaa ubingwa huo ikiwa na jumla ya pointi 86 ikifuatiwa na Real Madrid ambao wapo nafasi ya pili na pointi 84 huku Barcelona ya Lionel Messi ikiwa nafasi ya tatu na pointi 79 wakati timu iliyocheza na Suarez ikiwa nafasi ya 19 na pointi 31

Suarez amesema:”Barcelona hawakuweza kuonyesha thamani kwangu na Atletico Madrid walifungua njia kwangu. Nilikuwa ninafanya kazi kwa moyo na nilijitoa ndani ya klabu hii ambayo imekuwa ikiniamini,”.


SOMA NA HII  HAKUNA MCHEZAJI KAMA KANTE