Home epl CHELSEA YAPIGWA 2-1, YATINGA LIGI YA MABINGWA ULAYA

CHELSEA YAPIGWA 2-1, YATINGA LIGI YA MABINGWA ULAYA

 


WAKIWA Uwanja wa Aston Villa Park, ubao umesoma Aston Villa 2-1 Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England ambao ulikuwa ni wa mwisho leo kwa msimu wa 2020/21.

Ni Bertrand dakika ya 43 alipachika bao la kuongoza na lile la ushindi lilipachikwa na Anwar El Ghazi dakika 52 kwa mkwaju wa penalti.

Na Ben Chilwell alipachika bao dakika ya 70 kwa Chelsea huku Cesar Azpilicueta dakika ya 89 alionyeshwa kadi nyekundu.

Thomas Tuchel Kocha Mkuu wa Chelsea timu yake inamaliza ikiwa nafasi ya nne na pointi 67 na Aston Villa ipo nafasi ya 11 na pointi 55.

Licha ya kupoteza mchezo wa leo na kuacha pointi tatu ugenini, Chelsea itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa imemaliza msimu ikiwa ndani ya nne bora.


SOMA NA HII  ARGENTINA YENYE MESSI YAPETA COPA AMERICA 2021