Home Simba SC KICHAPO CHA MABAO 4-0 WALICHOPATA SIMBA CHAKWAMISHA FERRARI YA MO

KICHAPO CHA MABAO 4-0 WALICHOPATA SIMBA CHAKWAMISHA FERRARI YA MO


 BAADA ya kipigo ilichopata Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohammed Dewji Mei 16, 2021 aliamua kuwekeza fedha zaidi katika kuitengeneza Simba iweze kushindana zaidi.

Kikosi cha Simba leo Mei 17 kinatarajiwa kurejea Tanzania kikitokea nchini Afrika Kusini ambapo kilipoteza mchezo wake wa kwanza wa robo fainali kwa kukubali ubao usome Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Kupitia Twiter Mo aliandika:-“Nilipanga kujizawadia Ferrari na Rolls-Royce, sina budi kuweka mpango huu kapuni kwa sasa na kuelekeza fedha zaidi katika klabu yetu ya Simba SC Tanzania.

” Furaha ya Simba SC Tanzania ni muhimu kuliko starehe yangu. Simba kwanza!”.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa.


SOMA NA HII  TFF WAIPA SIMBA POINT 3 ZA 'MEZANI' KUTOKA JKT....ISHU NZIMA IKO HIVI....