Home Ligi Kuu KMC KAMILI GADO KUIVAA AZAM FC

KMC KAMILI GADO KUIVAA AZAM FC

 CHRISTINA  Mwagala, Ofisa Habari wa Klabu ya KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC. 

KMC inakumbuka kwamba imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara walipokutana Uwanja wa Majaliwa.

Azam FC wao mchezo wao wa mwisho wa ligi walikamilisha kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa na kusepa na pointi tatu mazima. 

Walipokutana mzunguko wa kwanza,  Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma KMC 1-0 Azam FC na kuwafanya Azam FC kuyeyusha pointi tatu jumlajumla. 

Mwagala amesema:”Tunahitaji kuwaoyesha Azam FC kwamba hatukufanya makusudi kuyeyusha Ice Cream katika mchezo uliopita, tupo imara na tunakwenda Azam Complex tukijiamini,” .

SOMA NA HII  NYOTA SITA WASIMAMISHWA NDANI YAPOLISI TANZANIA, RASHID JUMA WA SIMBA NDANI