Home epl KUMBE DE GEA ALIPUUZIA MBINU, KAFUNGWA PENALTI 40

KUMBE DE GEA ALIPUUZIA MBINU, KAFUNGWA PENALTI 40


KUMBE kipa namba moja wa Manchester United, David De Gea alipuuzia ushauri wa kocha wake wa makipa wa Manchester United kuhusu upigwaji wa penalti ambao mwisho wake umewafanya wafungwe na Villarreal katika fainali ya Europa League.

Iko namna hii baada ya dakika 120 kukamilika, De Gea alipewa karatasi ya maelekezo ya wapigaji penalti wote wa Villarreal ikionyesha upande wanaopendelea kupiga.

Lakini yeye akaipuuzia na mwisho wake hakudaka penalti hata moja kati ya 11 zote zilizama nyavuni jumlajumla.

Karatasi hiyo ilipatia baadhi ya mipigo ya wapinzani na iliandaliwa na Richard Hartsis lakini mwisho wa siku haikuwa na faida kwao.

Kufungwa kwa penalti hizo kunamfanya De Gea kushindwa kudaka penalti hata moja kati ya 40 ambazo amepigiwa akiwa langoni.

Mara ya mwisho kwa kipa huyo kudaka penalti ilikuwa ni miaka mitano iliyopita ambapo alizuia penalti ya Lukaku Romelu zama hizo akiwa Everton kufunga katika nusu fainali ya FA Cup, Aprili 23,2016.

Penalti hizo 11 alifungwa Mei 26 na kuwafanya wakose jumla taji la Europa League.

SOMA NA HII  SERGIO KUIBUKIA NDANI YA PSG