Home Yanga SC NYOTA TISA WAKOSEKANA YANGA YA NABI

NYOTA TISA WAKOSEKANA YANGA YA NABI


YANGA jana inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Katika mchezo huo, Yanga ilishinda ila haikuwa na nyota wake tisa ambao walikuwa nje kutokana na sababu mbalimbali.

Nyota hao ni pamoja na:- Yassin Mustapha yeye ni majeruhi aliumia alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania.

Carlos Carlinhos yeye ni majeruhi aliumia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons.


Abdallah Shaibu, ‘Ninja’ alipata majeruhi.

Saido Ntibazonkiza anasumbuliwa na majeruhi aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania.

Haruna Niyonzima huyu ana matatizo ya kifamilia.

Michael Sarpong ameenguliwa kikosini kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.

Lamine Moro yeye pia ameenguliwa kikosini kutokana na  utovu wa nidhamu.

Kipa namba moja Metacha Mnata naye pia ameenguliwa kikosini kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.

 Fiston Abdulazack yeye alipangwa kwa wachezaji wa akiba ila hakuwa eneo la uwanja kwa kile alichoeleza kuwa hajisikii vizuri kwa kuwa muda wa mechi alikuwa anazungumza na wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram. 
SOMA NA HII  YANGA YAPIGIA HESABU UBINGWA WA SIMBA