Home Yanga SC NYOTA WAWILI WA YANGA WAREJEA KIKOSINI

NYOTA WAWILI WA YANGA WAREJEA KIKOSINI


NYOTA wawili ambao ni chaguo la Mtunisia wa Yanga, Nasreddine Al-Nabi, Abdalah Shaibu ‘Ninja’, na kiungo wao kipenzi Carlos Carlinhos, ambaye pia aliumia hivi karibuni hatimaye kwa pamoja wamerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa takribani wiki tatu wakiuguza majeraha ya nyama za paja.

 

Mbali na hivyo, Ninja na Carlinhos kwa pamoja walikosa mechi tatu za timu hiyo, ikiwemo ile ya Namungo ambayo Yanga ilicheza ugenini na kutoka suluhu kisha mbele ya JKT Tanzania ambapo walishinda mabao 2-0 na Mwadui 0-2 Yanga kwenye Kombe la Shirikisho.


 Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema, Ninja na Carlinhos wamepona na kwamba tayari wameshaanza mazoezi.

 

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwajalia afya njema vijana wetu Ninja pamoja na Carlinhos na kubwa tumpongeze daktari wetu Nahumu Mganda kwa kusimamia matibabu yao vizuri.

 

“Hadi muda huu wanafanya mazoezi yao chini yake, hivyo baada ya wenzao kurejea kwenye ligi wataungana tayari kwa kuwa sehemu ya msaada kikosini,” alisema Bumbuli.


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  YANGA: MCHEZO MKUBWA HUCHEZWA NA WACHEZAJI WAKUBWA