Home Yanga SC CARLINHOS AWAPA MABAO MATATU YANGA, ANA KADI NYEKUNDU

CARLINHOS AWAPA MABAO MATATU YANGA, ANA KADI NYEKUNDU


NYOTA wa Yanga, Carlos Carlinhos amesepa Bongo akiwa amehusika kwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara kati ya mabao 43 huku akiwapa manahodha wake mabao matatu.

Mkataba wake wa miaka miwili ulivunjwa Mei 31 baada ya makubaliano ya pande zote mbili ambapo kwa sasa nyota huyo yupo zake nchini Angola.

 Sababu kubwa ya nyota huyo kuomba kuvunja mkataba inatajwa kuwa ni suala la msosi kuwa shida kwake hasa huu wa Tanzania tofauti na ule wa Angola.

Rekodi zinaonyesha kuwa alitoa pasi tatu za mabao na zote zilikutana na manahodha wake, pasi ya kwanza alitoa Uwanja wa Mkapa mbele ya Mbeya City alimpa nahodha Lamine Moro, Septemba 13, pasi ya pili alimpa Lamine, Uwanja wa Jamhuri, Moro, Septemba 27 mbele ya Mtibwa Sugar. Pasi ya tatu alitoa mbele ya Gwambina FC, Aprili 20 alimpa mshikaji Bakari Mwanyeto ambaye ni nahodha msaidizi.

Pia alitupia mabao matatu ambapo bao la kwanza alipachika Uwanja wa Mkapa mbele ya Coastal Union kwa pasi ya kiraka Deus Kaseke ilikuwa Oktoba 3.

 Bao la pili alifunga mbele ya Namungo FC kwa pasi ya Kibwana Shomari ilikuwa Uwanja wa Mkapa likuwa ni Novemba 22. Bao la tatu alifunga Februari 20 mbele ya Mtibwa Sugar kwa pasi ya Tuisila Kisinda, Uwanja wa Mkapa.

Amecheza jumla ya mechi 15 katika mashindano yote na alionyeshwa kadi moja nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.


SOMA NA HII  CAF WAZIPA TIKI YA BLUE SIMBA NA YANGA....MAMBO SASA NI 'BAMBAM'...