Home Uncategorized SIMBA MIKONONI MWA WAZIMBABWE KIMATAIFA

SIMBA MIKONONI MWA WAZIMBABWE KIMATAIFA


 BAADA ya Simba  kupenya hatua ya awali na kutinga hatua ya mtoano sasa inaingia mikononi wa Wazimbabwe kwenye hatua ya mtoano.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck jana Desemba 5 ililazimisha sare ya bila kufungana na Klabu ya Plateau United kutoka Nigeria Uwanja wa Mkapa.


Inapenya hatua ya mtoano kwa kuwa mchezo wa kwanza wa awali wa  Ligi ya Mabingwa uliochezwa Uwanja wa New Jos Nigeria Simba ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Clatous Chama.


Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 22-23 nchini Zimbabwe Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kati ya Januari 5-6.

SOMA NA HII  BREAKING:NIYONZIMA ASAINI YANGA