Home Simba SC KAMA ZALI VILE, TSHABALALA AINGIA ANGA ZA WASAUZI

KAMA ZALI VILE, TSHABALALA AINGIA ANGA ZA WASAUZI

 


HERRY Mzozo ambaye ni meneja wa beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema kuwa mchezaji huyo anawindwa vikali na klabu za kutoka nchini Afrika Kusini ‘Sauz’. 

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, beki huyo amefanikiwa kucheza michezo yote akianza kikosi cha kwanza.

Pia hata wakati Simba ikitwaa taji la kwanza la SimbaSuper Cup likiwa ni taji la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes aliweza kupata nafasi ya kucheza mechi hizo na kuonyesha kiwango kizuri.

Iliripotiwa kuwa, anatakiwa na Yanga ambayo inahitaji kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Mzozo alisema kuwa nyota huyo mkataba wake unakaribia kuisha na bado hajaongeza mkataba mwingine.

 “Tshabalala bado hajasaini mkataba na Simba, mkataba wake wa awali umesalia miezi miwili ili umalizike na kuna ofa kutoka katika timu za Afrika Kusini ambazo zimeonyesha nia kuwa zinamuhitaji.

“Kuhusu Yanga bado sijapata ofa rasmi, nasikia tu tetesi kuwa wanamhitaji.Lakini Simba bado wana nafasi kubwa ya kumuongezea mkataba kwa kuwa bado ni mali yao ila kama hizo timu kutoka Afrika Kusini zitafika makubaliano mazuri basi sisi hatutakuwa na shida, tutafanya biashara,” alisema meneja huyo.

Hivi karibuni kuhusu sakata hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Barbara Gonzalez, alisema:

 “Tunajua wazi kuwa beki na nahodha wetu Tshabalala mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari zipo timu ambazo zinavutiwa kumsajili lakini niweke wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba, lakini uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya ili aendelee kuitumikia klabu yetu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPATA USHINDI MKUBWA JANA....MATOLA AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA MAMBO YALIVYOKUWA UWANJANI..