Home Azam FC HUKO AZAM FC HAKUNA UTANI TENA

HUKO AZAM FC HAKUNA UTANI TENA

Azam FC

Kwenye mechi zao za ligi kwa kuweka wazi kuwa watendelea kasi yao ileile waliyoanza nayo kwenye mechi za ugenini.

Ipo wazi kuwa kwenye mechi mbili za ugenini Azam FC inayonolewa na Yusuph Dabo ilikomba pointi sita mazima ndani ya dakika 180.

Ilianza kushuhudia ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma ukisoma Mashujaa 0-3 Azam FC na kete ya pili ilikuwa Uwanja wa Highland Estate, Ihefu 1-3 Azam FC.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa bado hawajapoa wanahitaji kuendelea na kasi hiyo kwenye mechi zote.

“Bado tupo vizuri na benchi la ufundi linawapa mbinu wachezaji wetu kwa ajili ya mechi zote kuona kwamba tunapata ushindi hivyo tutazidi kupambana zaidi kwa ajili ya kupata pointi tatu.

“Ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua nasi tutaendelea kuleta ushindani kwa kuwa tuna timu bora yenye wachezaji ambao wanaleta ushindani mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

SOMA NA HII  KOCHA WA SINGIDA FOUNTAIN GATE AITAMBIA SIMBA, KAZI IPO HUKO TANGA