Home Simba SC SIMBA YAPENYA HATUA YA ROBO FAINALI MBELE YA KAGERA SUGAR

SIMBA YAPENYA HATUA YA ROBO FAINALI MBELE YA KAGERA SUGAR


LICHA ya Kagera Sugar kuanza kumtungua mapema kwa kichwa mlinda mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula dakika ya 45 kupitia kwa Eric Mwaijage ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa halikuweza kudumu mpaka mwisho wa mchezo.

Dakika 90 zilikamilka ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 2-1 Kagera Sugar na kuwafanya mabingwa hao watetezi wa taji la Kombe la Shirikisho kutinga hatua ya robo fainali.
Ni Bernard Morrison ambaye alipachika bao la kuweka usawa dakika ya 56 na lile la ushindi lilipachikwa na Meddie Kagere ambaye alitumia pasi mpenyezo ya Morrison.
Kipindi cha kwanza, Kagera Sugar walicheza kwa utulivu mkubwa huku wakiliandama lango la Manula ni kukosa utulivu kwa Vitalis Mayanga kulimfanya kukosa bao la wazi kipindi cha kwanza jambo ambalo atalikumbuka baadaye.

Kipindi cha pili Simba, Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu wa timu hiyo aliamua kubadili mbinu kwa kuwatumia washambuliaji wawili ambao ni Meddie Kagere na John Bocco ili kuongeza mashambulizi.

Kwa upande wa viungo aliamua kumuingiza Bernard ambaye aliweza kutimiza majukumu kwa wakati na kuwafanya Kagera Sugar washindwe kuhimili kasi ya wachezaji hao wanaowania taji hilo ambalo lipo mikononi mwao.

Kutinga kwao hatua ya robo fainali kunawafanya waungane na watani zao wa jadi Yanga ambao jana, Aprili 30 walitangulia baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.

 
SOMA NA HII  PABLO AAMUA LIWALO NA LIWE SIMBA...AWAPIGA CHINI SHIBOUB NA MOUKORO...'TRY AGAIN' ATOA KAULI...