Home news TFF YAFAFANUA JUU YA JINA LA HASSAN DILUNGA NA MUDATHIR

TFF YAFAFANUA JUU YA JINA LA HASSAN DILUNGA NA MUDATHIR


 BAADA ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen leo kutangaza orodha ya wachezaji 27 wa timu hiyo, imeelezwa kuwa nyota Hassan Dilunga alikuwa kwenye orodha ya kimaandishi kimakosa.

Orodha ya kwanza ilijumuisha wachezaji 27 na jina ambalo liliandikwa katika wachezaji hao ni pamoja na kiungo wa Simba, Hassan Dilunga.

Taarifa ambayo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa yalifanyika makosa katika uandishi.


“Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini Juni 5,2021. Kwa bahati mbaya katika kikosi kilichotolewa kwa maandishi kimeonesha mchezaji Hassan Dilunga ameitwa ikiwa ni makosa ya kiuandishi, Dilunga hajajumuishwa kwenye kikosi kama video inavyomuonesha kocha akitaja kikosi.

“Vilevile mchezaji Mudhathir Yahya ambaye ameitwa hakuonekana kwenye kikosi cha awali, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari, Cliford Mario Ndimbo.

SOMA NA HII  KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA...KABURU NJIA NYEUPEEE...KAZI ILIYOBAKI NI HII...