Home Yanga SC YANGA WATUA MTWARA KWA NDEGE

YANGA WATUA MTWARA KWA NDEGE

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi leo Mei 12 kimewasili salama Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Yanga wametua Mtwara na ndege ya Kampuni ya Precision Air ili kuanza kuwavutia kasi Namungo wanaonolewa na Hemed Morroco. 

Ni Mei 15 wanatarajiwa kukutana katika Uwanja wa Majaliwa ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 1-1 Namungo.

Miongoni mwa waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Wazir Junior, Farouk Shikalo na Metacha Mnata.



SOMA NA HII  YANGA: TULIPAMBANA CARLINHOS ABAKI MPAKA TUKAKODI WAPISHI