Home epl MANCHESTER CITY MABINGWA WA LIGI KUU ENGLAND

MANCHESTER CITY MABINGWA WA LIGI KUU ENGLAND


MANCHESTER City wamekuwa mabingwa wa Ligi Kuu England mara ya tatu katika misimu minne baada ya Manchester United kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wao waliokuwa nyumbani.

United usiku wa kuamkia leo ikiwa Uwanja wa Old Traford ilipoteza mchezo wao jambo lililowafanya waipe nafasi City kuweza kutangazwa kuwa mabingwa wakiwavua mabingwa watetezi Liverpool ambao kwa msimu huu mambo kwao yamekuwa magumu.

Ni Luke Thomas dakika ya 10 alipachika bao la kuongoza kwa Leicester City likasawazishwa na Mason Greenwood dakika ya 15 lile la ushindi lilipachikwa na Caglar Soyuncu dakika ya 66 na kuifanya Leicester kufikisha pointi 66 ikiwa nafasi ya tatu.

Manchester United ina pointi 70 huku vinara wakiwa ni Manchester City wakiwa na pointi 80 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani wao na Liverpool ipo nafasi ya 6 na pointi 57.

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola pia ana kazi ya kwenda kusaka taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo atakutana na Chelsea Mei 29 katika mchezo wa fainali.

Manchester City walikuwa wanatarajia kutwaa taji hilo wikendi iliyopita kwa kupata ushindi mbele ya Chelsea ila mambo yalikuwa magumu baada ya kupoteza mchezo huo.

.

SOMA NA HII  KISA USHINDI DHIDI YA HISPANIA...WAMOROCCO WAWAKANA WAARABU WENZAO...