MABOSI wa Shirikisho la Soka Ulaya, (UEFA) wapo tayari kuihamishia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley ila ikiwa Serikali ya Uingereza itakubali.
Uefa ilianza mipango hiyo hivi karibuni mara baada ya timu zote za nchi hiyo kufanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo husika.
Timu ambazo zimetinga fainali ya Uefa ni pamoja na mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City pamoja na Chelsea.
Inaelezwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alitarajiwa kukutana na Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin kwa ajili ya mjadala huo kwa kuwa Uturuki ambao walipewa tenda ya kuandaa walitajwa na Uingereza kama nchi hatarishi katika maambukizi ya Janga la Corona.