Home Yanga SC YANGA WATUA MTWARA, YAWEKA WAZI NAMUNGO SIO WEPESI

YANGA WATUA MTWARA, YAWEKA WAZI NAMUNGO SIO WEPESI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC hautakuwa mwepesi ila wapo tayari kwa ajili ya ushindani. 


Leo Mei 12 Yanga imetia timu Mtwara kwa ndege kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Mei 15, Uwanja wa Majaliwa.


Miongoni mwa wachezaji ambao wamewasili Mtwara ni pamoja na Lamine Moro, Faroukh Shikalo, Abdalah Shaibu, ‘Ninja, Deus Kaseke na Feisal Salum. 


Senzo Mazingiza ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuelekea katika mabadiliko ndani ya Yanga amesema kuwa wapinzani wao sio wa kuwabeza.


“Namungo ni timu imara hivyo mchezo wetu hautakuwa rahisi ila kutokana na kikosi tulicho nacho pamoja na mbinu za mwalimu kuna jambo la tofauti linaweza kutokea,”.

SOMA NA HII  MAKOCHA 72 WAOMBA KAZI YANGA