Home Azam FC JINA LA KIUNGO AZAM FC LAONDOLEWA STARS, MBADALA WAKE HUYU HAPA

JINA LA KIUNGO AZAM FC LAONDOLEWA STARS, MBADALA WAKE HUYU HAPA


WAKATI timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ikiwa imeanza mazoezi jina la kiungo Bryson Raphael mali ya Azam FC limeondolewa katika kikosi hicho.

Nyota huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji 27 walioitwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa Juni 13, Uwanja wa Mkapa.

Baada ya jina la nyota huyo kuondolewa mbadala wake ni nyota Yohana Mkomola anayekipiga ndani ya Vorskla Poltava ya Ukraine.

Taarifa kutoka kambi ya Stars zimeeleza kuwa Bryson baada ya kuwasili kambini alitoa taarifa kuwa ana majeraha ya kifundo cha mguu na kuomba aondolewe.


Chanzo: Spoti Xtra


SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC LEO KINACHOTARAJIWA KUANZA DHIDI YA SIMBA