Home Yanga SC MKUTANO MKUU YANGA : MANJI ATUA NA KUPAGAWISHA WANACHAMA

MKUTANO MKUU YANGA : MANJI ATUA NA KUPAGAWISHA WANACHAMA


MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji ameteka mkutano baada ya kuwasili katika ukumbi wa DYCC jijini Dar es Salaam kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo.

Manji aliwasili saa 11:07 asubuhi akiongozana na gari mbili, moja aina ya Nissan Xtrail na nyingine Toyota Land Cruiser.

Baada ya gari hizo kuwasili wanachama walikuwa hawajui yupo katika gari gani lakini Manji alishuka kwenye Nissan Xtrail na wanachama wakaanza kupiga shangwe.

Wanachama walimfungulia mlango na wakaanza kupiga nae picha huku yeye mwenyewe akionyesha kufurahi.

Manji alitoa nafasi kwa kila mwanachama aliyekuwa nje kupiga nae picha lakini makomandoo ndio walikuwa wanakataa.

Baada ya kumaliza kupiga picha na baadhi ya wanachama, Manji aliingia ndani na alianza kushangiliwa.

SOMA NA HII  KISA UBINGWA LIGI KUU...YANGA WATANGAZA HALI YA HATARI...