Home Yanga SC YANGA YATENGA BILIONI 7 ZA KUIVUA UBINGWA SIMBA SC MSIMU UJAO

YANGA YATENGA BILIONI 7 ZA KUIVUA UBINGWA SIMBA SC MSIMU UJAO


Klabu ya Yanga imetenga bajeti ya Sh7, 984, 406, 422 msimu wa 2021/2022.

Bajeti hiyo imetolewa kwa wanachama kwenye mkutano mkuu unaoendelea kwenye ukumbi wa DYCC, Dar es Salaam.

Katika bajeti hiyo, klabu ya Yanga imeainisha kukusanya Sh8, 149, 000, 000 kutoka kwenye udhamini, jezi, match day, social media na ada za uanachama.

Katika udhamini, Yanga imeanisha kukusanya Sh4, 901,736,274 wakati kwenye mapato ya jezi itakusanya Sh350 milioni.

Ada za wanachama klabu hiyo itakusanya Sh 2,040,000,000, match day Sh565 Milioni na kwenye social media Sh960 milioni.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KARIAKOO DABI...MANARA AWACHIMBA MKWARA WA KIMASAI SIMBA...