Home epl MOTO WA SALAH LIGI KUU ENGLAND NI BALAA

MOTO WA SALAH LIGI KUU ENGLAND NI BALAA


 MOTO wa nyota wa Liverpool, Mohamed Salah raia wa Misri umezidi kuwa wa kuotea mbali ambapo anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya Ligi Kuu England kwa msimu mmoja ambayo ni 32.

Ilikuwa ni msimu wa 2017/18 nyota huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu England ambapo la kwanza alitwaa akiwa na Klabu ya Chelsea na lile la pili alitwaa ndani ya Liverpool.

Mabao yake 32 yaliweza kuvunja rekodi za waliotangulia ambapo msimu wa 2013/14 alikuwa ni Luis Suarez, 2007/08 alikuwa ni Cristiano Ronaldo na Alan Shearer ilikuwa msimu wa 1995/96 hawa walitupia mabao 31 ndani ya msimu mmoja.

Pia Salah ni Mwafrika wa kwanza kuwa mfungaji wa muda wote ndani ya Liverpool katika UEFA akiwa na mabao 22 akivunja rekodi ya Steven Gerrad ambaye alitupia mabao 21. 

SOMA NA HII  MAJERAHA KUMUWEKA NJE POGBA NDANI YA MANCHESTER UNITED