Home Ligi Kuu RASMI..SIMBA NA YANGA KUPINGWA JUNI 10

RASMI..SIMBA NA YANGA KUPINGWA JUNI 10


Simba na Yanga zitapambana Juni  10 katika Fainali za  Ligi Kuu ya  vijana chini ya miaka 20 katika mchezo utakoafanyika Juni 10 kwenye uwanja wa  Azam Complex Chamazi

Timu hizo zimepangwa kundi  moja katika fainali hizo za vijana zitakazoanza Juni 10 hadi  19 kwenye uwanja wa Azam Complex.

Timu nane zimefuzu  Fainali hizo baada ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi  ambazo zilikua zinachezwa kwa muundo wa mechi za nyumbani na ugenini.

Timu zilizofunzu  katika nane bora ya Fainali hizo ni Yanga,Simba, Azam Mtibwa Sugar, Prisons, JKT Tanzania, Kagera Sugar na Mwadui .

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana liliendesha droo ya upangaji wa ratiba ya Fainali hizo ambapo Simba na Yanga zilijikuta zikiangukia

katika kundi A pamoja na  JKT Tanzania na Mwadui wakati kundi B lina timu za Azam, Kagera Sugar, Prisons na Mtibwa Sugar.

Ukiondoa mechi ya Simba na Yanga ambayo imepangwa kufanyika Juni 10 kuanzia saa 3:00 usiku pia kutakuwa na mchezo mwingine utakaoanza saa 1:00 usiku kati ya JKT Tanzania dhidi ya Mwadui.

Juni 11, Prisons itacheza na Kagera Sugar wakati Azam itapambana na Mtibwa Sugar huku mechi zote za Fainali hizo zikitarajiwa kufanyika usiku.

Nusu Fainali za Ligi hiyo zitafanyika Juni 17 wakati Juni 18 itakuwa i mapumziko wakati Fainali itafanyika Juni 19 itakayotanguliwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

SOMA NA HII  MWADUI FC KUIKOMALIA YANGA KWA MKAPA