Home Simba SC SIMBA KAMILI GADO KUMALIZANA NA RUVU SHOOTING

SIMBA KAMILI GADO KUMALIZANA NA RUVU SHOOTING


 SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Simba itashuka, Uwanja wa CCM Kirumba kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa.

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting na alikuwa ni Fully Maganga ambaye aliwatungua mabingwa hao watetezi.

Matola amesema:”Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting na tunaamini kwamba utakuwa mgumu ila tutapambana kupata pointi tatu.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunaendelea kupata ushindi kwani kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji pointi tatu na hilo lipo wazi,” amesema.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 64 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 10 na pointi 37.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zina hesabu tofauti kwa wakati tofauti.

Simba inahitaji kutetea ubingwa wa ligi huku Ruvu ikipiga hesabu kumaliza ndani ya tano bora.

SOMA NA HII  KAGERE, BOCCO NA MUGALU WAMPA KIGUGUMIZI GOMES ISHU YA USAJILI