Home EURO 2020 URENO YAVULIWA UBINGWA MAZIMA

URENO YAVULIWA UBINGWA MAZIMA

 MABINGWA watetezi wa taji la Euro 2020, timu ya taifa ya Ureno wamevuliwa taji lao rasmi baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa hatua ya 16 bora.

Bao la Thorgan Hazard dk 42 liliwafanya Ureno wakwame kulisawazisha mpaka dk 90 na kuwaacha wapinzani wao Ubelgiji wakitinga hatua ya robo fainali.

Ilikuwa ni Uwanja wa La Cartuja de Sevilla huko Hispania mwamba Cristiano Ronaldo aliweza kupiga mapigo huru mawili na yote hayakuweza kuipa bao timu yake hiyo iliyokuwa inapewa nafasi ya kutetea taji hilo. 

Nyota huyo anaweka rekodi ya kuwa mpigaji mapigo huru mara nyingi kuliko wachezaji wote ndani ya Euro tangu 2004 akiwa amepiga 28 na hajaweza kufunga bao lolote kupitia free kick. 

Wengine ni Andrea Pirlo, Darijo Srna, Deco hawa walipiga jumla ya free kick 7 huku wengine watatu walipiga 6.


SOMA NA HII  PERISIC ‘OUT’ CROATIA IKIWAVAA HISPANIA