Home Yanga SC YANGA YAWAITA MASHABIKI AZAM COMPLEX

YANGA YAWAITA MASHABIKI AZAM COMPLEX


UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti kubwa timu yao katika mchezo wao wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Juni 6 saa 1:00 usiku.

Mchezo huo utakuwa wa kirafiki ikiwa  ni lengo la Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi kuwaimarisha  wachezaji wake ambapo watamenyana na African Lyon. 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wajitokeze kuipa sapoti timu yao.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani tuna mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon utachezwa Uwanja wa Azam Complex, ” amesema. 

Kiingilio katika mchezo huo mzunguko ni 3,000 na VIP ni 5,000.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA MBEYA KWANZA...MASTAA YANGA WALA KIAPO...MAYELE ASHINDWA KUJIZUIA...