Home Simba SC SIMBA QUEENS WAPANIA KIMATAIFA

SIMBA QUEENS WAPANIA KIMATAIFA


 MABINGWA wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Simba Queens wameweka wazi kwamba wana imani ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Simba Queens kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) wanatarajia kukutana nao kwenye michezo ya kusaka tiketi ya kwenda Ligi ya Mabingwa wa Afrika.


Simba wanatarajia kwenda nchini Kenya kwa ajili ua mashindano hayo ambayo yataanza kufanyika Julai 17 hadi Agosti 1 jijini Nairobi na ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutoka wiki hii.

Meneja wa Simba Queens, Selemani Errasy Makanya amesema kuwa ana imani kwamba vijana wake wa watatwaa ubingwa wa Cecafa na kukata tiketi ya kwenda Champions League ambayo itafanyika baadae mwakani nchini Misri.

“Nina imani kuwa vijana wetu watanya vizuri na kutwaa ubingwa wa Cecafa na kupata tiketi ya kwenda ligi ya mabingwa kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira yetu,” alisema Makanya.

Simba waliingia kambini tangu Juni 17 na wamekuwa wakipiga tizi ili kujiweka tayari kwa mashindano hayo.

SOMA NA HII  BAADA YA KIPIGO KUPOA...KOCHA USGN AWACHANA SIMBA...ADAI ONYANGO NI TATIZO....ATOA ONYO...