Home Yanga SC YANGA: BADO HATUJAMALIZA LIGI, YATUMA SALAMU DODOMA JIJI

YANGA: BADO HATUJAMALIZA LIGI, YATUMA SALAMU DODOMA JIJI

 RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga ameweka wazi kuwa timu hiyo bado haijamaliza ligi hivyo katika mechi zao watakazocheza watapambana kupata pointi tatu. 


Kesho, Julai 18 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri,  Dodoma.

Mchezo wake uliopita kilishinda mabao 2-0 mbele ya Ihefu ambapo mabao yote yalifungwa na Feisal Salum


Tayari kikosi hicho kimeshatia timu Dodoma ilikuwa ni jana Julai 16 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda mabao 3-1 na kusepa na pointi tatu muhimu. 


Siwa amesema:”Bado tunaendelea kupambana na ligi kwetu haijaisha hivyo mechi zetu tutacheza kwa nidhamu tukihitaji ushindi,”.


Ikiwa nafasi ya pili na pointi 73 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 7 na pointi 43.

SOMA NA HII  FT: YANGA SC 4-1 SINGIDA BIG STAR....MAYELE AFANYA YAKE...KAGERE AENDELEA KUWACHOVYA YANGA...