Home news MSUVA:ILIKUWA NI MALENGO YANGU KUTWAA UBINGWA

MSUVA:ILIKUWA NI MALENGO YANGU KUTWAA UBINGWA


 KIUNGO mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya 
nchini Morocco, Simon Msuva, ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kubeba ubingwa wa ligi nchini humo, maarufu kwa jina la Botola Pro.


Nyota huyo amesema kuwa ilikuwa ni malengo yake kuona kwamba anaweza kutwaa ubingwa na timu hiyo.

Casablanca ilitangaza ubingwa huo baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wao Mouloudia Oujda mabao 2-0.

Msuva anaipa ubingwa huo Casablanca ukiwa ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge nao akitokea Difaa El Jadida ya nchini humo.

Ubingwa huo ni wa 21 ambao wameuchukua timu hiyo ambayo ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia msimu huu.

Kiungo huyo ameweka rekodi kubwa ambayo baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza na wanaocheza akiwemo Nickson Kibabag anayeichezea Club Athletic Youssoufi Berrechid ya nchini humo, wamempongeza.

Akizungumzia ubingwa huo, Msuva alisema: “Ni furaha kwangu kuweka historia yangu katika maisha ya soka kuchukua ubingwa hapa Morocco.

“Tangu najiunga na Casablanca haya yalikuwa malengo yangu ya kwanza kubeba ubingwa wa ligi kuu, licha ya kutamani zaidi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.”


SOMA NA HII  PAMOJA NA KUSAJILIWA AZAM FC MSIMU HUU...KIPA MFARANSA AINGIA TAMAA NA YANGA...AFUNGUKA A-Z ANAVYOITAKA ...