Home Yanga SC KIMEUANA: ZAWADI MAUYA AMSHUKIA MUKOKO KWA KUSABABISHA YANGA IFUNGWE

KIMEUANA: ZAWADI MAUYA AMSHUKIA MUKOKO KWA KUSABABISHA YANGA IFUNGWE


KIUNGO wa Yanga, Zawadi Mauya amefunguka sababu iliyowafanya washindwe kutamba tena dhidi ya Simba kuwa ni kucheza pungufu ndani ya dakika 45.

Yanga walimaliza pungufu baada ya kiungo mkabaji, Tunombe Mukoko kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi nahodha wa Simba John Bocco.

Amesema kipindi cha kwanza waliweza kumudu mcheza kadi nyekundu iliwatoa mchezoni kutokana na kucheza pungufu.

“Mchezo ulikuwa mguvu na wa preshak kila upande ulitaka kupata matokeo mapema kwa upande wetu hatukulewa ushindi wa mwisho dhidi ya wapinzani tuliingia kwakujiamini tukihitaji ushindi lakini haikuwa rahisi wapinzani wetu walijipanga pia,” amesema.

Mauya amesema wao walikuwa bora na wapinzani wao walikuwa bora washukukuru kadi hawakuwa wazembe hivyo walihitaji heshima lakini kukosa kwao matokeo wamechukulia kama sehemu ya mchezo amewapongeza Simba kwa kutwaa taji hilo huku akiwaambia kuwa wakutane msimu ujao.

SOMA NA HII  KATWILA AFUNGUKA KUHUSU MCHEZO WA YANGA