Home kimataifa ARSENAL YAMPIGIA HESABU LAUTARO

ARSENAL YAMPIGIA HESABU LAUTARO


 IMEELEZWA kuwa Klabu ya Arsenal ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez ili kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

Dau la kumpata nyota huyo ambaye bado ana mkataba ndani ya timu yake linatajwa kuwa ni pauni milioni 77 sawa na shilingi bilioni 246.6 kwa mkwanja wa ardhi ya Tanzania.

Katika orodha ya washambuliaji ambao wanahitajika ndani ya Arsenal yupo pia Tammy Abraham ambaye anakipiga ndani ya Chelsea kwa sasa na thamani yake inatajwa kuwa pauni milioni 40.

Sababu kubwa ya mshambuiaji huyo kuwekwa kwenye hesabu na Arsenal ni uhitaji wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mikel Arteta ambaye anataka kuipata saini ya raia huyo wa Argentina ambaye mkataba wake ndani ya Inter Milan una miaka miwili.

SOMA NA HII  DILI LA POGBA KUTUA JUVENTUS...'STATASI' YA LEO INASOMEKA HIVI...