Home Azam FC JEMBE JIPYA LAWEKA WAZI SABABU ZA KUMWAGA WINO AZAM

JEMBE JIPYA LAWEKA WAZI SABABU ZA KUMWAGA WINO AZAM


BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Azam, kiungo mshambuliaji Mzambia, Paul Katema ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya kukubali ofa ya Azam, ni kuvutiwa na uwekezaji mkubwa ambao klabu hiyo imeufanya kwenye miundombinu ya soka ikiwemo Uwanja wao wa Azam Complex.

Katema amejiunga na kutangazwa rasmi na Azam Juzi Alhamisi baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili na kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Azam akitokea klabu ya Red Arrows.

Katema anakuwa mchezaji wa tano mpya kutambulishwa na Azam kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22 ambapo watakuwa na ziada ya michuano ya kombe la Shirikisho, pamoja na michuano ya ndani.

AkizungumzIia usajili wake ndani ya Azam, Katema amesema: “Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kuwepo hapa, nimekuja kufanya kazi na kuongeza kiłe nilichonacho kwa ajili ya Azam. Nimesikia habari nyingi kuhusu timu hii kabla sijaja, na kujionea baadhi nilipokuja na Red Arrows kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

“Nilivutiwa sana na uwanja wao, na uwekezaji katika miundombinu ambayo kama klabu wamefanikiwa kuwa nayo, na ndiyo maana sikusita kukubali ofa yao.”

SOMA NA HII  AZAM FC WAIMBOMBOA MBEYA CITY MBELE YA FAMILIA ZAO...PIRA LA KOCHA MPYA LAINUA MATUMAINI MAPYA...