Home Ligi Kuu KMC V SIMBA, TAMBO ZATAWALA WOTE WANASAKA POINTI TATU

KMC V SIMBA, TAMBO ZATAWALA WOTE WANASAKA POINTI TATU


 LEO Uwanja wa Mkapa saa 1:00 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya KMC v Simba, unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Ikumbukwe kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-0 KMC hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa KMC na Simba wakihitaji kusepa na pointi tatu muhimu baada ya kupoteza mchezo wao uliopita mbele ya Yanga.

Kocha wa Klabu ya KMC Habibu Kondo amesema kuwa malengo yao ni kupata ushindi ili kuendelea mbio za kumaliza ndani ya nne bora katika msimamo. 

KMC inatafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, ikiwa imekusanya pointi 42 mpaka sasa kwenye michezo 32 iliyocheza huku ikiwa nafasi ya sita. 

Kondo amesema:”Tunajua ni vigumu kucheza na timu iliyotoka kupoteza kwenye Derby na ukizingatia ni timu inayotetea ubingwa, hivyo tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha mipango yetu kama tunavyotarajia.”

Nahodha Msaidizi wa  kikosi cha KMC Mohamed Samata amesema kuwa wanahitaji kupata alama tatu muhimu ili kuendelea kusaka tiketi ya kucheza michuano ya kimataifa mwakani. 

“Tanzania kuingiza timu nne ni fursa kwetu kuhakikisha na sisi tunakuwa miongoni mwa hizo timu nne mwakani,” . 

Kwa upande wa Simba, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Selemani Matola amesema kuwa wanafahamu wanahitaji alama tatu ili kutangaza ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

“Tunahitaji alama tatu ili tuweze kuwa mabingwa wa ligi na tunaimani tunaanza leo ijapokuwa tuliteleza kwenye Derby, tunaiheshimu KMC lakini tunaimani na kikosi chetu. “

Alli Salim kipa namba tatu wa kikosi hicho amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanatangaza ubingwa kabla ya ligi kumalizika kama mashabiki wao wanavyotarajia na wamesahau kichapo cha mchezo wao uliopita.



SOMA NA HII  NAMUNGO YATAMBIA USAJILI WAO MPYA