Home Yanga SC MZEE MPILI AUGUA GHAFLA DAR, AREJEA IKWIRIRI

MZEE MPILI AUGUA GHAFLA DAR, AREJEA IKWIRIRI


HAJI Omari ‘Mzee Mpili’ amezua hali ya sintofahamu, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa kifua.

Mzee Mpili aliugua Jumatano akiwa nyumbani kwake Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani, lakini kesho yake alipata nguvu ya kufuata milioni yake aliyoahidiwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kama Yanga ikiifunga Simba.

Kwa muhibu wa meneja wa Mzee Mpili amesema kuwa kweli Alhamisi alichukua mzigo wake huo na kurejea zake Ikwiriri ambako inaelezwa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

 

Mzee huyo alijipatia umaarufu mkubwa katika mchezo kati ya Simba na Yanga, baada ya kudai kuwa ‘aliutengeneza’ mchezo huo kwa faida ya Yanga, na kweli wakashinda 1-0 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Mzee Mpili, Mohamed Mkilalu, alisema kuwa: “Mzee amerejea Ikwiriri baada ya kwenda Dar kuchukua fedha zake kwa Haji Manara.

 

“Manara alimpa ahadi ya milioni moja endapo Yanga itaifunga Simba, kwa hiyo alimkodia usafiri wa kwenda na kurudi.


“Ni kweli alikuwa anaumwa kifua lakini sasa hivi anaendelea vizuri baada ya kutumia dozi ambazo amepewa na daktari.”


SOMA NA HII  KISA FEI TOTO KUHUSISHWA NA AZAM FC....YANGA SC WAPANGA KUSUSIA BIDHAA ZA AZAM...