Home Azam FC WATATU WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA LEO AZAM COMPLEX

WATATU WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA LEO AZAM COMPLEX


 NYOTA watatu wa Azam FC leo Julai 15 wanatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ila kuna baadhi ya wachezaji ambao watakosekana.

“Kila kitu kipo sawa ila kuna wachezaji ambao tutawakosa ikiwa ni pamoja na Sure Boy pamoja na Agrey Morris hawa wanaumwa pia bado hali ya Prince Dube haijawa kwenye ubora.

“Kwa upande wa maandalizi tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kuona kwamba tunapata pointi tatu, mashabiki watupe sapoti,” ,

Azam FC mchezo wao uliopita wa ligi mbele ya Simba ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-2 hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya pili na pointi zake ni 64 inakutana na Simba ambao wametangazwa kuwa mabingwa wakiwa na pointi 79.

Dube ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Azam FC akiwa ametupia mabao 14 na pasi tano za mwisho.

SOMA NA HII  SAKATA LA WACHEZAJI AGGREY MORRIS, SURE BOY KUSIMAMISHWA...TFF WAISHUKIA AZAM FC...