Home Simba SC YANGA MMEISHAAAH…GOMES ATUMIA DK 5 KUMTIA ‘NDIMU’ MORRISON

YANGA MMEISHAAAH…GOMES ATUMIA DK 5 KUMTIA ‘NDIMU’ MORRISON


KUELEKEA mechi ya Ligi Kuu kati ya watani wa jadi Simba na Yanga Julai 3, kocha mkuu wa Simba Didier Gomes ameonekana akikomaa kutoa maelekezo kwa winga Benard Morrison katika mazoezi ya timu hiyo leo.

Katika mazoezi hayo yanayofanyika jioni hii ya leo Julai Mosi kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, baada ya timu hiyo kufika uwanjani na kupiga dua, wachezaji wengine walijitenga katika kundi moja huku Morrison akibaki na Gomes katikati ya kiwanja.

Wawili hao walifanya mazungumzo kwa muda usiopungua dakika tano, kisha wakaungana na wachezaji wengine waliokuwa wakipiga stori za pamoja.

Baada ya hapo wachezaji wote wamejikusanya sehemu moja na kuanza kucheza kwa kupigiana pasi fupi fupi huku wengine wakikaba mchezo uliozoeleka kwa jina lisilo rasmi la ‘Zubaisha bwege’.

Wakati huo huo makipa wanne wa timu hiyo, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim na kinda mwingine kutoka timu ya vijana walionekana kuendelea na programu yao maalumu.

Katika mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi kuanzia saa 11:00 za jioni, Simba ndio watakuwa wenyeji ikiwa ni mchezo wa duru ya pili baada ya ule wa kwanza Yanga wakiwa wenyeji kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS vs YANGA PRINCESS KITAUMANA TENA KESHO....JE JWANGANI WATAIONEA TENA MSIMBAZI?