Home Simba SC LUIS MIQUISSONE HUYO KUIBUKIA KWA WAARABU, DILI LAKE MIAKA MINNE

LUIS MIQUISSONE HUYO KUIBUKIA KWA WAARABU, DILI LAKE MIAKA MINNE

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imekubali ofa ya dola za Marekani 900,000 (zaidi ya Tsh Bilioni 2) kumuuza kiungo mshambuliaji wake Luis Miquissone.

Raia wa Msumbiji aliwapa tabu mabosi wa Klabu ya Al Ahly ya Misri walipokutana nao kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa aliwatungua bao moja akiwa nje ya 18.

Nyota huyo kuna uwekezako mkubwa msimu ujao akwa kwa Waarabu hao wa Misri ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tayari Simba na Ahly wamefikia makubaliano hayo ambapo Miquissone amekubali kujiunga na Al Ahly kwa mkataba wa miaka minne.


Kutokana na dili la kiungo huyo mwenye kasi awapo uwanjani huku mguu wake wa kushoto ukiwa ni pendwa kwake tayari Simba wamempa dili la miaka mitatu Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wake.

SOMA NA HII  NYOTA WATATU WACHUNIWA SIMBA ISHU YA KUONGEZA MKATABA