Home Simba SC RASMI, SIMBA YAINASA SAINI YA KIUNGO KUTOKA MALI KWA TSH MILIONI 300

RASMI, SIMBA YAINASA SAINI YA KIUNGO KUTOKA MALI KWA TSH MILIONI 300


RASMI leo Agosti imemtambulisha kiungo aliyekuwa anakipiga ndani ya Al Ahly Benghazi ya Libya, Sadio Kanoute mwenye umri wa miaka 24 kuwa mali mpya ya kikosi hicho.

Anajiunga na mabingwa watetezi ambao wameweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dau ambalo anatajwa kupewa nyota huyo ni zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya usajili wake na ni dili la miaka mitatu ambayo anatajwa kusaini.

Ni kiungo mwenye uwezo wa kukaba na kushambulia ikiwa atapewa nafasi na uwezo wake ukajibu ndani ya Simba inayonolewa na Didier Gomes.

Kiungo huyo amesema kuwa ni furaha kwake kujiunga na Simba hivyo atafanya juhudi kutimiza majukumu yake.


SOMA NA HII  KUHUSU TETESI ZA CHAMA KUSEPA SIMBA...MAGORI KAIBUKA NA HILI ZITO..."NDIO KWANZA TUMEANZA"..