Home Yanga SC EHEE..BEKI MPYA YANGA KUMBE NI KIMEO..APIGWA MARUFUKU KECHEZA..

EHEE..BEKI MPYA YANGA KUMBE NI KIMEO..APIGWA MARUFUKU KECHEZA..


Yanga itawakosa mabeki wake wawili wa kusoto Yassin Mustapha na ingizo jipya David Bryson lakini taarifa ni kwamba wanatakiwa kupona kwanza sawasawa na majeraha yao madogo.

Mabeki hao walipata maumivu katika nyakati tofauti kabla hawajatua hapa ambapo Yassin aliumia msimun uliopita huku Bryson akipata maumivu kabla ya Yanga kumsajili akiwa na KMC.

Yanga imewapeleka mabeki hao katika vipimo toafuti tena wakiwa hapa Morocco na wakitakiwa kupumzika, kidogo na kufanya mazoezi mepesi tofauti na wenzako kwa wiki mbili.

Maabeki hao leo wamekuwa wakiwa nje ya Uwanja huku Bryson pekee alikuwa akifanya mazoezi ya kutembe nje ya uwanja huku Yassin akiwa anafuatulia mazoezi hayo sambamba na kiungo Mapinduzi Balama.

Daktari wa Yanga Youssef Ammir amesema wachezaji hao wataanza mazopezi taratibu kulingana na jinsi vipimo vilivyoonyesha ambapo wote wanasumbuliwa na tatizo la nyama.

“Tumewafanyia vipimo jana na leo tumeanza na Bryson kuanza akianza taratibu lakini hawa wengine nao tutawafuatilia taratibu jinsi wanavyondelea hatutawakimbiza sana watakuwa nje kwa muda kidogo.”

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA WALIVYOICHANGAMSHA CAF KIBABE...UMAARUFU WAPANDA KWA KASI...