Home Uncategorized ARSENAL YAMPIGIA HESABU BEKI WA DORTMUND

ARSENAL YAMPIGIA HESABU BEKI WA DORTMUND


BEKI wa Klabu ya Borussia Dortmund, Manuel Akanji inaripotiwa kuwa ameingia kwenye anga za Klabu ya Arsenal ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Licha ya Janga la Virusi vya Corona kutingisha dunia na kutikisa uchumi wa timu nyingi za Ligi Kuu England bado Arsenal inampango kabambe wa kuboresha kikosi chao.

Ubora wa beki huyo ulionekana kwenye mchezo wa Bundesliga wikeendi ambapo Dortmund iliwanyoosha Schalke kwa mabao 4-0 jambo ambalo limezidi kuwavuta Arsenal kwa beki huyo mwenye miaka 24.

Arsenal iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta inapiga hesabu kumpata beki huyo ambaye mkataba wake unameguka msimu wa 2022.

SOMA NA HII  MBWANA SAMATTA AWEKA REKODI HII ENGLAND