Home Uncategorized ALEX SONG AELEZA ALIVYOFUATA MKWANJA BARCELONA ANUNUE FERRARI

ALEX SONG AELEZA ALIVYOFUATA MKWANJA BARCELONA ANUNUE FERRARI





Kiungo Alex Song amekiri kuwa kikubwa ambacho kilimpeleka Barcelona akitokea Arsenal ni kwa kuwa aliahidiwa mshahara mkubwa na akaona ni nafasi kubwa ya yeye kuwa tajiri.

Alitua Barcelona kwa pauni 15m mwaka 2012 baada ya kudumu Arsenal kwa miaka sita. Mshahara wake ulipanda kutoka pauni 55,000 hadi 70,000 kwa wiki. 

“Kabla ya kusajili niliambiwa sitacheza mechi nyingi, ofa yao ilipokuja sikufikiria mara mbili, nilikuwa na ndoto ya kuendesha Ferrari.

“Nilipofika Arsenal… ile nafika mazoezini nikaona usafiri wa mfalme (Thierry Henry), ulikuwa niwa hatari, nikajiambia na mimi nataka nifike levo zake, ndiyo maana ilipotokea nafasi sikuzubaa,” alisema Song.

SOMA NA HII  SIMBA YAIPIGIA HESABU KALI AZAM FC