Home kimataifa JACK GREALISH MZEE WA KUVUNJA REKODI

JACK GREALISH MZEE WA KUVUNJA REKODI

 

KWA sasa Jack Grealish ni mali ya Manchester City na amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Sergio Arguero ambaye yupo Barcelona akiwa ni mzee wa kuvunja rekodi. 

Alikuwa ndani ya Aston Villa msimu uliopita. Ndani ya Ligi Kuu England alicheza jumla ya mechi 97 mabao 15 na pasi 19 za mabao.

Katika mashindano yote amecheza jumla ya mechi 295 amefunga mabao 43 na pasi 59 za mabao.

Yeye ni kiungo mshambuliaji aliletwa duniani Septemba 10,1995 ana umri wa miaka 25 na urefu wake ni m 180.

Mguu wake anaopenda kuutumia mara nyingi ni ule wa kulia ambao anapenda kuutumia akiwa uwanjani.

Mbali na kuwa kiungo mshambuliaji pia anaweza kucheza nafasi ya winga wa upande wa kulia.

Thamani yake ya pauni milioni 100 ambayo ni ada ya usajili imevunja rekodi ya Paul Pogba wa Manchester United ambaye alisajiliwa kwa zaidi ya pauni milioni 93.


SOMA NA HII  IHEANACHO AENDELEA KUWABEBA LEICESTER