Home Azam FC LWANDAMINA: TUNAREJESHA UTIMAMU WA WACHEZAJI

LWANDAMINA: TUNAREJESHA UTIMAMU WA WACHEZAJI

[the_ad id="25893"]


GEORGE Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika mchezo wa kirafiki dhidi Red Arrows. 

Kwenye mchezo huo wa kurejesha utimamu wa mwili Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 huku Lwandamina akiweka wazi kuwa kuna jambo ameliona kwa wachezaji wake.

“Nilikuwa nataka kuona wachezaji wanarejea katika utimamu wa mwili hasa kutokana na uchovu pamoja na kukaa muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani.

“Hata namna wachezaji walicheza bado walionekana hawajawa tayari hivyo taratibu wanarejea katika hali ya kawaida ni jambo la kusubiri,” amesema. 

Azam FC imeweka kambi nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na itawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  AZAM FC V KMC NI SAA 1:00 USIKU, MUDA WABADILISHWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here