Home kimataifa MESSI AKUBALI KUSAINI MIAKA MIWILI, PICHA YAKE YAONDOLEWA

MESSI AKUBALI KUSAINI MIAKA MIWILI, PICHA YAKE YAONDOLEWA


LIONEL Messi amekubali kujiunga na Klabu ya Paris Saint-Germain kwa dili la miaka miwili.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or mara sita leo amesafiri mpaka  Paris kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na timu hiyo ya Ufaransa.

Messi inelezwa kuwa alikuwa na ofa kibao baada ya kuondoka Barcelona lakini yeye amechagua kwenda PSG.

Tayari wafanyakazi wa Barcelona wameanza kazi ya kuiondoa picha yake kubwa iliyokuwa kwenye Uwanja wa Nou Camp hivyo ni rasmi kwamba utawala wake umemeguka ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 34 ni mfungaji bora wa muda wote ndani ya Barcelona anakwenda kuungana na mshikaji wake wa kitambo Neymer Jr.



SOMA NA HII  KITENDO CHA KUIFUNGA ARGENTINA TU...SAUDI ARABIA WAMEVUNJA NA KUWEKA REKODI HIZI KIBAO...