Home Simba SC MUGALU AINGIA ANGA ZA RS BERKANE YA MOROCCO

MUGALU AINGIA ANGA ZA RS BERKANE YA MOROCCO


 IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu yupo kwenye rada za Klabu ya RS Berkane ya Morocco ambayo inafundishwa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge.

Ibenge anamtambua Mugalu kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ule anaifundisha AS Vita ya Congo.

Kwenye mchezo wa hatua ya makundi walipokutana Congo, Mugalu aliyeyusha furaha ya AS Vita kwa kufunga bao kwa penalti na aliwasumbua mabeki wa timu hiyo jambo ambalo limemfanya akubali uwezo wake.

 Ikiwa mambo yatakwenda sawa huenda dili hilo likamiliziwa nchini Morocco kwa kuwa Klabu ya Simba imepanga kwenda huko kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

SOMA NA HII  CHIKWENDE KUVUNJIWA MKATABA SIMBA, KAHATA MAMBO BADO