Home Yanga SC YANGA KUANZA KUTANGAZA MAJEMBE MAPYA

YANGA KUANZA KUTANGAZA MAJEMBE MAPYA


UONGOZI wa klabu ya Yanga umekuja na utaratibu rasmi wa kuwatambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili, kwa ajili ya kuwatumia kwa msimu ujao wa 2021/22 ambapo tayari kupitia utaratibu huo wamemtambulisha mshambuliaji wao mpya, Fiston Mayele.

Yanga mpaka sasa inatajwa kumalizana na baadhi ya wachezaji wakiwemo aliyekuwa mlinzi wa AS Vita, Shaban Djuma, kipa wa Aigle Noir Erick Johola, mshambuliaji, na wingwa wa Dodoma Jiji, Dickson Ambundo.

Baadhi ya wachezaji hao wapya wa Yanga wanatarajiwa kutumika kwenye michuano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), inayoanza kutimua vumbi rasmi leo Jumapili kwa mchezo mmoja utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumzia utaratibu huo, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema: “Tunaendelea na mchakato wa kuboresha kikosi chetu kupitia dirisha hili la usajili, ili kuzidi kuwa na kikosi bora zaidi kwa ajili ya msimu ujao.

“Kuhusiana na kuwaweka wazi nyota hao wapya ambao tayari wamekamilisha usajili, kuna utaratibu rasmi unamaliziwa kuandaliwa ili kuwaweka wazi nyota hao.”


 

SOMA NA HII  "AZIZ KI AMTEKETEZA CHAMA" MCHAMBUZI...AMEFUNGUKA HAYA A-Z