Home kimataifa BRUNO AKOMALIA ISHU YA KUPIGA PENALTI

BRUNO AKOMALIA ISHU YA KUPIGA PENALTI


 LICHA ya kukosa penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wakati timu ya Manchester United ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Aston Villa nyota wa timu hiyo Bruno Fernandes amesema kuwa ataendelea kupiga penalti kama kawaida.

Bruno penalti yake ilipaa juu ilikuwa dakika ya 90 na kufanya United wapoteze pointi tatu jumlajumla kwenye mchezo wao huo uliochezwa Uwanja wa Old trafford.

Nyota huyo amewaomba msamaha mashabiki kwa kusema kuwa imani yake atapata nafasi ya kufunga tena kwa sababu kukosa ni jambo la kawaida.

“Hakuna mtu ambaye ameumia zaidi yangu kutokana na kukosa penalti hii na pia timu yangu kuchapwa, nimekuwa nikiamini kuwa ni jukumu langu na nimekuwa nikifanya kwa ukamilifu.

“Leo nimeshindwa, lakini ninataka kukuhakikishia kuwa nitaendelea kupiga penalti mashabiki wategemee hilo siku zijazo,” .

SOMA NA HII  DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA